MKEKA WAKO, MACHAGUO YAKO

ACCA Generator Bure

Chagua siku, market, idadi ya mechi na total odds unazotaka, kisha bonyeza “Tengeneza mkeka”.

Tengeneza mkeka wako

1 Chagua siku

Mechi ambazo hazijaanza pekee. Saa ni za Tanzania (EAT).

2 Chagua market

Unaweza kuchagua zaidi ya moja.

Over / Under 1.5
Over / Under 2.5
1X2
BTTS
First half

Mechi 2–10
Mechi moja, pick moja.

Tutajaribu total odds kati ya 2.70–3.30 (±10%). Zisipopatikana, tutakupa idadi ya mechi ulizochagua kwa odds tofauti na kukuambia.

Bure. Hakuna akaunti inayohitajika.

Mkeka wako

Mkeka wako utaonekana hapa

Weka machaguo yako, nasi tutatafuta mechi zinazolingana na total odds unazotaka.

Mechi ulizochagua, odds zilizo wazi

Tunatumia odds za bookmaker zilizohifadhiwa. Kila mechi huingia mara moja, na total odds hupatikana kwa kuzidisha odds za picks zote.

Odds zinaweza kubadilika. Hakikisha odds na kickoff kwa bookmaker wako kabla ya kuweka bet.

Jinsi ACCA Generator inavyofanya kazi

ACCA, au accumulator, ni mkeka wenye picks za mechi kadhaa. Chagua siku ya mechi, market unazopendelea, idadi ya mechi na total odds. Generator hutafuta mchanganyiko unaolingana na machaguo yako kwenye odds zilizohifadhiwa.

  1. Chagua siku. Leo, Kesho au Kesho kutwa. Mechi ambazo tayari zimeanza hazijumuishwi.
  2. Chagua market. Over 1.5, Over 2.5, Under, Home Win, Away Win, BTTS, HT Over 0.5 au HT Under 1.5. Ukichagua market kadhaa, mkeka unaweza kuzichanganya; si lazima kila market iingie.
  3. Weka idadi ya mechi. Tumia vitufe vya − na + kuchagua mechi 2 hadi 10. Kila mechi ina pick moja tu.
  4. Weka total odds. Kwa odds 3.00, tunatafuta mkeka wenye total odds 2.70 hadi 3.30. Zisipopatikana, tunajaribu idadi ya mechi na market ulizochagua bila kikomo cha total odds, kisha kukuonyesha ujumbe na odds halisi. Odds za picks huzidishwa, hazijumlishwi.
  5. Tengeneza na beti mkeka. Angalia picks, odds na kickoff. Bonyeza “Beti Mkeka Huu” kufungua Betway kwenye tab mpya, kisha chagua picks hizi kuweka bet. Unaweza pia kutengeneza mkeka mwingine bila kubadili machaguo yako.

Market hizi zina maana gani?

Over / Under huhusu jumla ya magoli ya mechi. Kwenye 1X2, unaweza kuchagua Home Win au Away Win. BTTS: Yes inahitaji timu zote mbili kufunga; BTTS: No inahitaji angalau timu moja isifunge. HT Over 0.5 inahitaji angalau goli moja kipindi cha kwanza. HT Under 1.5 inahitaji kipindi cha kwanza kiishe na magoli 0 au 1.

Angalia mkeka kabla ya kuweka bet

Hakikisha market, odds na kickoff kwa bookmaker wako. Mkeka wa accumulator unahitaji picks zote kushinda. Mechi yoyote inaweza kutoa matokeo tofauti na matarajio.

Generator haitoi booking code wala kuweka bet kwa niaba yako. Mkeka hautangazwi au kuhifadhiwa kwenye VIP. Tumia kiasi unachoweza kumudu kupoteza.

Maswali kuhusu ACCA Generator

Je, kutengeneza mkeka ni bure?

Ndiyo. Unaweza kutengeneza mkeka bila kuingia kwenye akaunti.

Kwa nini total odds hazilingani kabisa na nilizoandika?

Odds za mechi zilizopo haziwezi kutoa kila jumla kwa usahihi. Tunajaribu tofauti ya ±10% kwanza. Lengo lisipopatikana, tunakupa idadi ya mechi ulizochagua bila kikomo cha total odds. Ujumbe kwenye mkeka unaeleza kilichobadilika, na total odds halisi zinaonekana wazi.

Kwa nini hakuna mkeka uliopatikana?

Tutakuambia sababu: hakuna odds kwa siku hiyo bado, mechi zimeanza, odds za market hazijakamilika, mechi zinazofaa hazitoshi, au hakuna mkeka mwingine wenye mechi mpya. Punguza idadi ya mechi, chagua market nyingine au badili siku kulingana na ujumbe. Kubadili total odds pekee hakusaidii kama mechi zinazopatikana hazitoshi.

Je, mkeka mwingine utakuwa na mechi tofauti?

Kwa machaguo yaleyale, angalau mechi moja lazima itofautiane na mkeka uliotengenezwa mara iliyopita. Mikeka inaweza kufanana kwa baadhi ya mechi. Kama hakuna mwingine unaolingana, tutakuambia.

Je, mkeka uliotengenezwa unahakikisha ushindi?

Hapana. Mechi yoyote inaweza kutoa matokeo tofauti na matarajio. Mkeka wa accumulator unahitaji picks zote kushinda.